Thursday, 22 February 2018

TASAF YAWA CHACHU YA KUBORESHA MAISHA YA WAKAZI WA KABUNGU



Bi. Agnes akionyesha mafanikio yake baaada ya Tasaf kumsaidia

Wanufaika 
wa mradi wa tasaf kata ya kabungu iliyopo katika wilaya ya Tanganyika wameishukuru serikali kwa kuwaletea mradi ambao umewasaidia kuboresha maisha yao.
 Wameyasema hayo walipozungumza na mpanda radio na kusema kuwa maisha waliyokuwa nayo zamani hayakuweza kukidhi mahitaji yao ukilinganisha na sasa walivyoingizwa katika mradi huo.

Mradi wa tasaf ulianzishwa mwaka 2014 ambao ulikuwa na lengo la kunusuru kaya masikini ambazo hazina uwezo wa kukidhi mahitaji muhimu  ya kijamiiambayo ni  elimu,maradhi na chakula.

Vijiji 170 vipo kwenye mpango wa mradi huo na vijiji 80 tu ndivyo vilivyonufaika na mradi huo mpaka sasa mkoani Katavi.
bwana maulid akiwa mbele ya nyumba aliyoboresha baada ya kupata manufaa kupitia tasaf
Source:Furaha Kimondo


No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...