Mkuu wa wilaya ya tanganyika Salehe Muhando |
Wilaya ya Tanganyika inakabiliwa na tatizo la uhaba wa shule za
sekondari hali inayopelekea kushusha kiwango cha ufaulu mkoani katavi.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya hiyo salehe muhando wakati wa kipindi
cha majadiliano katika kikao cha 11 cha
kamati ya ushauri mkoa.
Aidha amesema uhaba wa shule za kata imekuwa chanzo cha kutengeneza
mazingira ya utoro na kuiomba ofisi ya elimu mkoa kuonyesha ushirikiano ktk
jitihada zinazotoka kwa wazazi na wilaya hiyo.
Wilaya ya Tanganyika iliyopo mkoani katavi ina kata 16 huku ikiwa na
shule za kata sekondari 8 pekee.
Source Restuta
Nyondo
No comments:
Post a Comment