picha kiwanda cha kusindika maziwa katavii |
Vijana
mkoani katavi wametakiwa kutumia fursa ya mazingira ili kuendana na sera ya
Tanzania ya viwanda ili kukabiliana na tatizo la ajira nchini
Wito
huo umetolewa leo na mkurugenzi wa kiwanda cha kusindika maziwa cha Katavi
Diary bwana Gabriel Lunguya wakati cha kilichopo mtaa wa kasimba wakati
akizungumza na mpanda radio ofisini kwake
Amesema
kila mzalishaji anayo nafasi ya kushinda soko la bidhaa zake endapo atajikita
katika uzalishaji wa bidhaa zenye ubora
Akizungumzia
fursa za ajira tangu kuanzishwa kwa kiwanda hicho zaidi ya miezi Bwana Lunguya mamesema mpaka sasa kimeajiri
vijana watatu kwenye ajira rasmi na wengine zaidi ya 100 kwenye ajira zisizo
rasmi
Katika
hatua nyingine amewataka vijana kujiamini na kuthubutu kuwekeza katika sekta
mbalimbali ili kunyanyua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla
Source:Haruna Juma
No comments:
Post a Comment