Pichani walimu wa mkoa wa katavi |
Baadhi ya walimu katika halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoani
Katavi,wamesema wanasubiri kuona serikali inatekeleza agizo lake la kulipa
madeni ya walimu mwezi huu.
Wamesema miongoni mwa athari zitokanazo na kutolipwa mishahara na
stahiki nyingine kwa wakati ni pamoja na kudhorotesha ufanisi katika kazi
pamoja na kusababisha ugumu wa maisha kwao.
Mara kadhaa,chama cha Walimu Mkoani Katavi kimekuwa kikipaza sauti ya
kuitaka serikali ilipe madeni na sahiki nyingine za walimu ili kuchochea
utendaji kazi shuleni.
Mwezi uliopita,serikali ilisema katika kipindi cha mwezi Februari
mwaka huu,italipa madeni ya walimu na watumishi wengine wanaoidai serikali.
Source Issack Gerlad
No comments:
Post a Comment