Sunday, 11 February 2018

Baadhi ya wafanyabiashara wanaofanyia biashara zao soko la mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi maarufu kama Machinga wameulalamikia uongozi wa soko hilo kwa kuwasitisha kufanya biashara maeneo waliyokuwepo hali inayopelekea kurudisha nyuma maendeleo

MPANDA

Wakizungumza na Mpanda Redio wamesema uongozi haukutoa maelekezo yoyote tangu kusitishwa kwa biashara na kudai kuwa licha ya  kufuatilia kwa uongozi husika wameambiwa wanaotakiwa kufanya biashara ni wale wote walio na vibanda

Viongozi wa soko hilo Elisha Chang’ombe  ambaye ni Makamu Mwenyekiti na bw Sharubu Issa katibu wa soko hilo wamesema kuwa wafanyabiashara waopanga bidhaa zao chini  ndio wanaokwepa ushuru  hali ambayo inasababisha kukosekana kwa mapato

Wafanyabiashara hao wameomba uongozi husika kuendelea  kufanyia biashara zao maeneo hayo  kwani ndio maeneo rafiki na biashara wanazozifanya. 

Chanzo:Mpanda Radio
#Changia Damu Okoa Taifa

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...