NSIMBO
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha
Kapanda halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wameutuhumu uongozi wa kijiji hicho
kwa kushindwa kushughulikia utatuzi wa tatizo la uhaba wa maji safi na salama.
Kwa kiasi kikubwa wahanga wa tatizo hilo wakiwa ni wanawake wameiambia Mpanda radio, kuwa muda mwingi unatumika kutafuta maji kuliko kufanya shughuli za kimaendeleo.
Mmoja wa viongozi Bw Maiko Chananza amekiri kuwepo kwa tatizo hilo huku akizitupia lawama mamlaka zingine kwa kushindwa kuwajibika.
Sera ya maji ya taifa inataka
maeneo ya vijijini maji yapatikane kila umbali wa mita 400 jambo ambalo mpaka
sasa limebaki na utata.
Chanzo:Mpanda Radio
#Changia Damu okoa Taifa
No comments:
Post a Comment