DAR ES SALAAM
Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, imedai maandalizi yanaendelea
vizuri kwa uchaguzi mdogo wa marudio katika Jimbo la Kinondoni, Siha na Kata nane
ikiwa pamoja na kutatua changamoto ndogo ndogo
zinazojitokeza.
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi
Bw. Ramadhani Kailima amesema hayo mara baada ya kikao na watendaji wa tume
kabla ya uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika jumamosi ijayo (Februari 17).
Mkurugenzi huyo amesema kuwa
tume imejipanga kuanza kutoa vipindi vya elimu ya mpiga kura mfululizo hadi
siku ya uchaguzi, elimu ambayo itakua ikigusia mada mbalimbali za uchaguzi
ikiwemo haki na wajibu wa mpiga kura, wakala wa vyama vya siasa na msimamizi wa
uchanguzi.
Chanzo: Eatv
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment