Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa |
DAR ES SALAAM
Mjumbe wa Kamati Kuu ya
Chadema na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa amewapongeza maaskofu kwa
kuunga mkono mambo aliyosema wamekuwa wakiyapigania.
Lowassa ametoa pongezi hizo wakati akimnadi
mgombea ubunge jimbo la Kinondoni, Salum Mwalimu katika Kata ya Kijitonyama.
Baraza la Maaskofu Katoliki
Tanzania (TEC), limetoa ujumbe wa Kwaresima wa mwaka 2018 ndani yake likitoa
msimamo kuhusu masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii nchini.
Ujumbe huo ulioandikwa na
maaskofu wote 35 wa TEC wakiongozwa na Rais wake, Mhashamu Tarcisius
Ngalalekumtwa upo katika kitabu cha kurasa 20 ikiwa ni maandalizi ya ibada hiyo
ya siku 40, kipindi ambacho ni cha mfungo wa sala kukumbuka siku 40 za Kristo
kufunga na kwenda jangwani.
Chanzo:Mwananchi
#Changia Damu Okoa Taifa
No comments:
Post a Comment