Tuesday, 24 October 2017

Xi Jinping: Kiongozi mwenye nguvu zaidi nchini China tangu kipindi cha Mao Zedong'.



Chinese President Xi Jinping raises his hand as he takes a vote at the closing session of the 19th National Congress of the Communist Party of China at the Great Hall of the People, in Beijing, China 24 October 2017.Haki miliki ya picha
Image captionBw Xi alishiriki kupiga kura Jumanne
Chama cha Kikomunisti nchini China kimepiga kura kujumuisha falsafa zake Xi Jinping katika katiba na kumuinua hadi kifikia kiwango alichokuwa nacho mwanzilishi Mao Zedong.
Kura hiyo ya kuunga mkono kuandika fikra zake Xi Jinping, ilifanyika wakati wa kukamilika kwa mkutano mkuu wa chama cha Kikomunisti ambao ndio mkutano mkubwa zaidi wa kisiasa nchini China.
Bw. Xi ameongeza madaraka yake tangu ashike uongozi mwaka 2012.
Hatua hiyo ni ishara kuwa wapinzani wake hawawezi kumpinga bila ya kitishia utawala wa chama cha Kikomunisti.
Chinese minority delegates wearing traditional costumes arrive for the closing ceremony of the 19th National Congress of the Communist Party of China (CPC) at the Great Hall of the People (GHOP) in Beijing, China, 24 October 2017Haki miliki ya picha
Image captionZaidi ya wajumbe 2,000 kutoka China wamekuwa wakikutana
Mkutano huo wa Komunisti ulianza wiki iliyopita kwa hotuba ya saa tatu ya Bw. Xi. ambapo alielezea falsafa yake ya siasa za ujamaa.
Maafisa wa vyeo vya juu na vyombo vya habari vya serikali walianza kuzungumzia falsafa hiyo wakiitaja kuwa fikra zake Jinping, ishara kuwa Bw. Xi alikuwa ameimarisha ushawishi wake chamani.
Watoto wa shule, wanafunzi wa vyuo vikuu na wafanyakazi katika makampuni ya serikali sasa wataungana na wanachama milioni 90 wa chama cha Kikomunisti, kusoma fikra zake Xi Jinping kuhusu kipindi kipya cha ujamaa.
Souvenir plates with images of Chinese late Chairman Mao Zedong and Chinese President Xi Jinping are seen at a shop during the ongoing 19th National Congress of the Communist Party of China, in Beijing, China 21 October 2017.Haki miliki ya picha
Image captionMabadiliko ya katiba yanamweka Xi Jinping (kushoto) kiwango sawa Mao Zedong (kulia)
Ikiwa kwanza alikuwa ni mwenyekiti Mao kuunganisha nchi ambayo ilikuwa imeharibiwa na vita na ya pili, ya China kutajirika nchini ya Deng Xiaoping, kipindi hiki kipya ni cha kujenga umoja zaidi na wakati huo huo kuifanya China kwa na nguvu nje.
Kuyajumuisha haya yote kwa jina la Xi Jinping kwenye katiba ya chama ina maana kuwa washindani hawawezi kupinga Xi, bila ya kutishia chama cha Kikomunisti.
Zaidi ya wajumbe 2,000 walitumia mkutano huo wa wiki nzima kuwachagua wakuu wa chama mikoani, magavana na wakuu wa mashirika yanayomilikiwa na serikali.
@habari na bbc swahili

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...