Friday, 2 June 2017

Wakazi Wadai Fidia Chuo Cha Veta Mpanda Kwa Miaka Kumi

Na, Tizibazomo Bernard
Wakazi wapatao 31 wenye zaidi ya ekari 340 za ardhi kuzunguka chuo cha Veta Mpanda wamelalamikia maeneo yao kuchukuliwa na chuo kwa zaidi ya miaka kumi sasa bila kulipwa fidia na wakizuiliwa kufanya  shughuli za kiuchumi.


Wakizungumza wamesema kuwa chuo hicho kiliahidi kuwalipa fidia baada ya tathimini ya maeneo hayo kukamilika lakini wameshindwa kufanya hivyo na wamekuwa hawapati ushirikiano kutoka kwa viongozi.

"Waturudishie maeneo yetu ili tuendelee kulima wakiwa tiyari watakuja tena kwa kuwa ni mpango wa serikali," "kinachotushangaza ni kuwa sisi tumekatazwa kulima ila wao wanayakodisha mashamba yetu huku sisi bado tunaangaika na njaa bora waturudishie mashamba" walisema wananchi hao

Wananchi hao wamedai kuwa kama chuo hicho hakijawa tiyari, kiwarudishie maeneo yao waendelee kulima mpaka hapo watakapokamilisha taratibu za malipo ya fidia.

"Wakikukuta shambani mwako hata kama ulikuwa unatafuta Mpini utasikia weka panga chini mimi nikasema mniue na panga langu, wakasema haya haraka bibi ondoka tumechukua na picha yako ole wako urudie, sasa mimi na umri huu hawataki kunipa hela yangu wanasubiri kuja kunipa lini."Aliongeza Bibi Mmoja

Vingozi wanaokaimu Ofisi ya chuo hicho waligoma kuongelea kwa undani suala hilo wakidai mwenye Mamlaka ya kuliongelea Ni Mkuu wa chuo ambaye yupo nje ya ofisi.


alipotafutwa Mkuu wa Chuo hicho Bwana Matagane kwa njia ya simu alisema kuwa hawezi kuongelea suala hilo na kusema walio ofisini ndio wanapaswa kuliongelea.
"ni kweli nipo safarini lakini Mkuu wa chuo anaposafiri ofisi ya Mkuu wa chuo haisafiri, mumuone anayekaimu ofisi awaeleze kuhusu suala hilo" alisema Matagane.
viongozi wanaokaimu ofisi pamoja na kufwatwa tena lakini majibu yao yalikuwa ni yaleyale.
"suala hili anayeweza kulizungumzia na anayejua undani wa suala lenyewe ulipofikia ni mkuu wa chuo." alieleza Afisa mmoja ambaye hakutaja jina lake.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...