Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu |
JERUSALEM
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema
kuwa wapalestina ni lazima wakubali kuwa Jurusalem ndio mji mkuu wa Israel ili
amani iweze kupatikana.
Netanyahu amesema Jerusalem umekuwa mji mkuu wa
Israel kwa miaka 3,000 na haujakuwa mji mku wa watu wengine.
Amesema hayo huku maandamano yakiendelea kwenye
ulimwengu wa kiislamu kufuatia hatua ya Marekani kuutambua Jurusalem kuwa mji
mkuu wa Israel.
Ghasia zimezuka karibu na ubalozi wa Marekani
nchini Lebanon na kwingineno siku ya Jumapili.
Akiongea mjini Paris baada ya mazungumzo na rais
wa Ufaransa Emmauel Macron, Bw Netanyahu amesema kuwa jitihada za kuwanyima
wayahudi mji wa wa Jerusalem ni kitu kibaya.
Chanzo: Dw swahil
No comments:
Post a Comment