Kisha polisi wakaandamana na mwanamume huyo hadi kwa nyumba moja
iliyo mtaa wa KwaZulu-Natal, ambapo sehemu zaidi za miili ya binadamu
zilipatikana.Wanaume wanne, wawili kati yao madaktari wa kitamaduni walikamatwa
na kushtakiwa kwa mauaji au kupanga kuua.
Walifikishwa katika mahakama ya Estcourt kilomita 175 kaskazini
magharibi mwa mji wa Durban.kuwa
wanaume hao wanne walio na umri wa kati ya miaka 22 na 32 ni sehemu ya genge
kubwa.
Uchunguzi bado unaendelea na polisi wamewashauri watu ambao jamaa
zao wametowewa kujitokeza.Wachunguzi wa visa vya uhalifu wameitwa kutambua sehemu hizo za
binadamu, kwa kuwa haijulikana ikiwa sehemu hizo ni za mtu mmoja au watu
kadhaa.
Mwezi mmoja uiopita mjini Durban, mwanamume mmoja alikamatwa akiwana
na kichwa cha binadamu ambacho inanamiwa alikuwa na mpango wa kikiuza kwa
daktari ya kitamadunia.
No comments:
Post a Comment