Halmashauri ya wilaya ya Mpanda mkoani katavi
imetenga eneo la Luhafwe kwa ajili ya uwekezaji ili kufikia Tanzania ya viwanda.
Yamesemwa hayo na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri
ya Mpanda Bwn Rojas Romuli alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake kwa lengo la kutolewa ufafanuo uwekezaji huo na jinsi walivyojipanga
kuhakikisha wanafanikiwa katika mipango hiyo.
Mkurugenzi Romuli amesema “kuwa tayari wameshatenga
eneo la hekta 2400 ambapo kuna eneo kwa ajili ya ufugaji,kilimo,utalii,suma
JKT,huduma za kijamii ,biashara pamoja na makazi ya watu.”
Aidha amesema tayari wameshapima viwanja kwa ajili
makazi na vitatolewa kwa shilingi laki moja kwa kaya na kila kaya itapewa
hekari mbili za kulima bure.
Hata hivyo mkurugenzi aliendelea kusema lengo
kuu ni kuhifadhi Ardhi na mazingira na kuyatumia katika namna ambayo ni
endelevu kwa matumizi ya vizazi vya sasa na baadae.
No comments:
Post a Comment