Monday, 20 November 2017

Wanafunzi 21 wa kidato cha tano na sita shule ya sekondari ya St. Paul Liuli wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kufanya uhalifu kwa kuharibu miundombinu.



 
Wanafunzi 21 wa kidato cha tano na sita shule ya sekondari ya St. Paul Liuli wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma
RUVUMA

Wanafunzi 21 wa kidato cha tano na sita shule ya sekondari ya St. Paul Liuli wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kufanya uhalifu kwa kuharibu miundombinu. 

Wanafunzi hao ambao waliungana kufanya uhalifu huo majira ya saa tatu za usiku, walianza kwa kuzima mifumo ya umeme shuleni hapo na kisha kufanya uvamizi wa kupasua vioo vya madirisha ya shule pamoja na kupiga mawe. 


Mkuu wa wilaya ya Nyasa, Bi. Isabela Chilumba ametembelea na kukagua uharibifu uliofanywa na wanafunzi hao katika shule hiyo, hata hivyo kamati ya ulinzi na usalama ilivyokagua bweni la wanafunzi hao walikuta wakiwa na silaha zenye ncha kali ikiwemo visu, mapanga, nondo, karata pamoja na bangi huku akiagiza bodi ya shule ichukue hatua kali dhidi yao

SOURCES:EATV

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...