Monday, 20 November 2017

Hospitali 10 za Serikali zilizoonyesha jitihada za kuokoa maisha ya mama na mtoto zimekabidhiwa mashine za Utrasound zenye thamani ya Sh143 milioni.



 

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salam,  Mheshimiwa Paul Makonda

DAR ES SALAAM

Hospitali 10 za Serikali zilizoonyesha jitihada za kuokoa maisha ya mama na mtoto zimekabidhiwa mashine za Utrasound zenye thamani ya Sh143 milioni.

Hospitali hizo zimepatiwa mgao wa mashine hizo za kisasa aina ya GE Vscan Access ni Amana, Mwananyamala, Mnazi Mmoja, Buguruni, Kimara, Tandale, Temeke, Sinza, Mbagala Rangi Tatu na Vijibweni.

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salam, Paul Makonda amewapongeza wauguzi na madaktari walioko mstari wa mbele kuokoa maisha ya mama na mtoto.

Amesema uchaguzi wa vituo hivyo ulizingatia viashiria vya utendaji vilivyowekwa kwenye hospitali 22 zinazosaidiwa na mradi wa kujenga uwezo wa CCBRT.

Mshauri wa kiufundi wa mradi wa kujenga uwezo wa CCBRT, Dk Brenda Sequeira amesema Mpango huu wa kuzipatia hospitali mashine za Utrasound ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa miaka saba wa kuwajengea uwezo watumishi wa afya na kuboresha miundombinu ya afya

SOURCES:MWANANCHI

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...