TFDA |
DODOMA.
Kaimu meneja wa TFDA kanda ya kati Mkoa wa dodoma Englberth Bilashoboka amewataka watumiaji wa bidhaa za vyakula kutoa taarifa mapema kwenye ofisi ya mganga mkuu popote alipo kama kuna bidhaa zilizofungiwa, zilizoharibika na zisizo na kiwango ambazo zinawafikia wananchi.
Bilashoboka ameyasema hayo mjini Dodoma na kusisitiza kuwa kama kuna mfanyabiashara yeyote anayesambaza bidhaa zisizo na ubora au zilizokwisha muda wa matumizi atoe taarifa mapema mahali husika.
Aidha amewataka wanunuzi wa bidhaa kukagua kwa uangalifu kabla ya kuinunua na kuitumia ili kujiepusha na madhara yatokanayo bidhaa ambazo muda wa matumizi yake kumalizika.
Bilashoboka amewaasa watengenezaji kuwa na alama maalumu ili watengenezaji wengine wasiige bidhaa yake .
Mbali na hayo amesema sheria kali zitachukuliwa kwa yeyote ambaye atasambaza bidhaa zisizo na ubora kwa wanunuzi na watumiaji.
No comments:
Post a Comment