NAIROBI
Mahakama
ya Juu nchini Kenya imetupilia mbali kesi zilizofunguliwa na wafuasi wa NASA za
kupinga ushindi wa Urais wa Uhuru Kenyatta, kwenye uchaguzi wa marudio wa
Oktoba 26, 2017
Kesi
hiyo ambayo ilikuwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari, iliongozwa na
majaji 6 akiwemo Jaji Mkuu David Maraga, na kutoa uamuzi kuwa Uhuru
Kenyatta ni mshindi halali wa uchaguzi wa Oktoba 26.
Kufuatia
uamuzi huo wa mahakama ya Juu nchini Kenya, Uhuru Kenyatta anatarajiwa
kuapishwa wiki ijayo, na kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa muhula wa pili.
Ikumbukwe
uchaguzi wa marudio ulifanyika baada ya Mahakama ya Juu kufuta matokeo ya Urais
ya uchaguzi wa kwanza wa Agosti 8, 2017 na kutaka urudiwe mara ya pili
No comments:
Post a Comment