Mkazi mmoja wa kijiji
cha weka ngombe katika kata ya katuma wilaya ya Tanganyika Juma Abubakari
amevamiwa na kuuawa na watu wasio julikana akiwa nyumbani kwake.
Akithibitisha kutokea
kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa katavi Benedikti Mapujila
amesema tukio hilo limetokea majila ya saa nne usiku Mnamo tarehe 4/5/2018 nyumbani
kwa marehemu alipokuwa amekaa na familia
yake ghafla alivamiwa na watu wasio julikana na kutekeleza tukio hilo.
Aidha amesema kuwa
upelelezi wa tukio hilo unaendelea na
mara baada ya upepelezi wa kipolisi kukamilika jeshi hilo litatoa taarifa kwa
umma kuhusiana na tukio hilo.
Ametoa wito kwa wanachi
kushilikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu
katika maeneo yao ilikuendelea kuimarisha hali ya usalama.
Chanzo:Paul
Mathias
No comments:
Post a Comment