Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Stalike Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi wamesema majibu wanayopata kutoka kwa viongozi baada ya kuwahoji juu ya uwajibikaji hayako katika utendaji kwa asilimia zote.
Wakizungumza na Mpanda Radio kijijini hapo wamesema mara
kadhaa huwahoji juu ya masuala
mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na huduma za kijamii na migogoro
ya ardhi.
Diwani wa kata ya stalike Adam Chalamila amesema wananchi
wanapewa fursa ya kuhoji juu ya maendeleo
japo suala la migogoro ya ardhi
bado linaendelea kufanyiwa kazi ili wakazi hao wafahamu hatma yao baada
ya katazo la serikali kulima katika maeneo ya hifadhi.
Kwa mujibu wa Diwani Chalamila wakazi walioathirika zaidi na
migogoro ya ardhi ni kutoka katika Kijiji cha Stalike,Igongwe na Matandalani.
Chanzo:Ester Baraka
No comments:
Post a Comment