DAR ES SALAAM
Kamati Kuu ya Chama cha Demokarasia na Maendeleo Chadema
imemaliza Vikao vyake na kufikia uamuzi wa kushiriki kwenye uchaguzi mdogo katika
majimbo ya Kinondoni na Siha unaotarajiwa kufanyika Februari 19 mwaka huu.
Baada ya uamuzi huo kamati kuu imewateua wagombea wa Majimbo
hayo ambapo Mhe.Salum Mwalim Juma ameteuliwa kugombea jimbo la Kinondoni huku
Bw. Elvis Christopher Mosi akiteuliwa kugombe jimbo la Siha.
Kwa mjibu wa John Mrema ambaye ni Mkurugenzi wa
Itikadi,Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, Wagombea wote wameshachukua
fomu za uteuzi kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye majimbo husika.
Wagombea hao wanatajia kurejesha fomu hizo kesho leo kwa
ajili ya uteuzi.
Chanzo:Mpekuzi
Blog
No comments:
Post a Comment