RUKWA
Wanafunzi wakiume wilayani
Nkasi Mkoani Rukwa wameonywa
kuacha tabia kuanzisha lugha zenye kupelekea vitendo vya ngono wawapo
shuleni
Wito huo umetolewa na
afisa elimu Sekondari wilayani Nkasi Abel Ntupwa katika kikao kazi cha kuboresha taalumu kilichowajumuisha
Wakuu wa shule 23 za sekondari wilayani humo.
Kufuatia hali hiyo
amedai kuwa ni marufuku kwa mtu yeyote
kumwita mtoto wa kike ambaye ni Mwanafunzi majina ya kimahaba ili
kuwaweka Watoto hao katika hali ya usalama.
Kwa upande wake afisa
elimu wa mkoa wa Rukwa Nestory Mloka amesema yeye binafsi kamwe hawezi kusita
kuwavua madaraka Walimu wakuu ambao wataonyesha kushindwa kuzisimamia shule zao
ili zitoe matokeo chanya.
Chanzo:Rukwa Kwanza Blog
No comments:
Post a Comment