MARA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kassim Majaliwa amesema Serikali imekataza kilimo cha pamba cha mkataba kwa
sababu kinawanyonya wakulima.
Ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi baada ya
kukagua zahanati ya Hunyari wilayani Bunda akiwa katika ziara ya kikazi mkoani
Mara.
Amefafanua kuwa
Serikali imeweka mkakati wa kuimarisha mazao makuu ya biashara ambayo
uzalishaji wake umeanza kupungua likiwemoa zao la pamba.
Aidha Waziri Mkuu amesema
Serikali imeamua kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa kilimo cha zao la
pamba kuanzia hatua za maandalizi ya shamba,pembejeo hadi masoko.
Katika hatua nyingine amesema
Serikali itachukua hatua kali za kisheria kwa mfugaji yeyote atakayelisha
mifugo yake katika mashamba ya wakulima kwani tabia hiyo huchangia migogoro
baina yao.
Chanzo:Mpekuzi
No comments:
Post a Comment