NEW YORK
Marekani imeitaka Pakistan
kutoyapa hifadhi makundi yale inayoyataja
kushiriki katika vitendo vya kigaidi.
Majibizano hayo yametokea katika Baraza la Usalama wakati wa mkutano
kuhusu mahusiano ya Afghanistan na majirani zake wa Asia ya Kati pamoja na
masuala ya amani na usalama.
Naibu Waziri wa Mambo ya nje
wa Marekani John Sullivan amesema Marekani haiwezi kufanya kazi pamoja na
Pakistan wakati ikiendelea kuyapatia hifadhi makundi ya kigaidi na imeitaka
iache kufanya hivyo na kuunga mkono juhudi za kutatua mgogoro wa Afghanistani.
Kwa upande wake Pakistan imeutaka
utawala wa Rais Donald Trump kushughulikia maeneo yanayolinda magaidi nchini
Afghanistan pamoja na pato lao linalotokana na biashara ya madawa ya kulevya.
Chanzo:Dw swahili
No comments:
Post a Comment