Saturday, 20 January 2018

Chama tawala cha ZANU-PF nchini Zimbabwe kimetangaza kuwafukuza wabunge wake 11 ambao ni washirika wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe


HARARE

Chama tawala cha ZANU-PF nchini Zimbabwe  kimetangaza kuwafukuza wabunge wake 11 ambao ni washirika wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Robert Mugabe.

Maamuzi ya kuvuliwa uanachama wabunge hao yametolewa na kutangazwa Bungeni na Naibu Spika wa Bunge la Zimbabwe, Mabel Chinomona baada ya Bunge hilo kupokea barau kutoka kwenye chama cha ZANU PF iliyosema wabunge hao wamefukuzwa kwa mujibu wa Katiba ya Zimbabwe kupitia kifungu namba 129 (1) (k).

Naibu Spika amesema kuwa wabunge waliofukuzwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani, aliyekuwa Waziri wa Nishati, aliyekuwa Waziri wa Michezo, aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na wabunge wengine wa majimbo mbalimbali nchini humo. 

Kufuatia zoezi hilo Bunge limetangaza nafasi wazi katika majimbo hayo 11 na kuijulisha Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe kuhusu uwepo wa nafasi za wazi katika majimbo hayo kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo ili zoezi la uchaguzi liweze kufanyika kupata wawakilishi wa Wananchi. 


Chanzo:Dw swahili

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...