Friday, 19 January 2018

Wakulima wa zao la Tumbaku wa Chama Cha Msingi Cha Ukonongo katika halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wamelalamikia kucheleweshewa malipo ya zao la tumbaku katika msimu wa mwaka uliopita.

Picha na zao la Tumbaku

MLELE

Wakulima wa zao la Tumbaku wa Chama Cha Msingi Cha Ukonongo katika halmashauri ya Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi wamelalamikia kucheleweshewa malipo ya zao la tumbaku katika msimu wa mwaka uliopita.

Wakizungumza na Mpanda redio kwa nyakati tofauti wamesema licha ya mchanganuo wa malipo kufanyika bado wakulima wengi hawajapatiwa fedha zao hali ambayoinasababisha ugumu wamaisha katika msimu huu wa kilimo .

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho cha msingi Godfley Malilo amesema changamoto iliyopo ni uingizwaji wa ushuru wa chama umecheleweshwa lakini hatua za kuanza malipo hayo yanatarajiwa kuaanza wiki ijayo.

Chama hicho cha msingi kinawakulima wa tumbaku zaidi ya elfu mbili na kimekuwa kikichangia kwa kiasi kikubwa katika pato la halimshauri ya wilaya ya Mlele.

Chanzo: Paul mathius 

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...