Takribani watu 41 wanaotoka katika kijiji cha
kampuni kata ya misunkumilo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi
wanatarajia kupata elimu ya watu wazima MEMKWA kutokana na kutopata fursa ya
kupata elimu mapema.
Mwenyekiti wa kijiji hicho James Saimoni
amebainisha hayo wakati akizungumza na mpanda redio kuhusiana na jitihada za
ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi nsambwe yatakayosaidia kuongeza chachu ya watoto
kupata elimu mapema.
Amesema shule hiyo ina jumla ya walimu watatu
pekee walioajiriwa na serikali hivyo kuwalazimu wanakijiji kutafuta walimu
wengine wakujitolea kwa ajili ya
kuwafundisha wanafunzi hao.
Shule ya msingi sambwe haijakamilisha usajili
kutokana na mapungufu ya vyumba vya madarasa pamoja na matundu ya vyoo.
CHANZO:Ester Baraka
No comments:
Post a Comment