Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu
Raphael Muhuga ameeleza kusikitishwa na wazazi ambao hawajawapeleka shuleni
watoto waliofaulu mtihani na kutakiwa kujiunga na masomo ya sekondari kidato
cha kwanza mwaka 2018.
Muhuga ameelezea masikitiko yake wakati
akifungua vikao vya wadau wa elimu
ufunguzi ambao umefanyika katika uwanja wa Azimio Halmashauri ya
Manispaa ya Mpanda ili kujadili pamoja na kutatua vikwazo vinavyosababisha Mkoa
wa Katavi ushike kitaaluma katika ufaulu wa wanafunzi.
Aidha Mkuu wa Mkoa ametoa kiasi cha shilingi
laki tano kwa ajili ya kusaidia kumalizia miundombinu ya shule ya msingi
Mtakumbuka ikiwa ni baada ya mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Augustino Paul
Filimbi kusema shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa,vyoo vya
walimu na wanafunzi.
Vikao vya wadau wa elimu ambavyo vimezinduliwa
jana,vinatarajia kufikia kilele chake Aprili 16 mwaka huu katika kijiji cha
Majimoto Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele ambapo leo vikao hivyo vimeendelea
katika Halmashauri ya Nsimbo.
Chanzo:Isack Gerald
No comments:
Post a Comment