Wito
umetolewa kwa idara ya maendeleo ya
jamii kutoa elimu ya kutosha kwa
wanawake na vijana kujiunga katika vikundi
ili waweze kufaidika na asilimia 10 inayotengwa na halmashauri.
Hayo
yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi
halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Samson Medda wakati akizungumza na
mpanda na kusema kuwa maafisa maendeleo ya jamii wanapswa kutoa elimu hiyo ili
wananchi waweze kupata uelewa ili kuweza
kupata mkopo huo na kuwezesha kupunguza umaskini.
Aidha
amesema kuwa licha ya kuwezesha baadhi ya vikundi vya vijana na wanawake
serikali ina mpango wa kuongeza kundi la walemavu kuingia katika uwezeshwaji wa
mikopo hiyo katika mwaka wa fedha licha
kumekuwa na changamoto katika urejeshaji wa fedha hizo kwa wakati.
Mpaka
kufikia mwezi march mwaka huu Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika imetoa fedha
kutoka katika mapato ya ndani kiasi cha
shilingi milioni mia moja kumi na tisa kwaajili ya kuwezesha vikundi vya
wanawake na vijana.
Chanzo:Restuta Nyondo
No comments:
Post a Comment