Wednesday, 4 April 2018

MUHUGA ATOA AGIZO KALI KWA WADAU WA ELIMU KATAVI



Mkuu wa mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga amewagiza watendaji mbalimbali Wakiwemo Wakuu wa shule na kamati zake mkoani Katavi kuhakikisha wanasimamia vizuri elimu ili kuondoa tatizo la wanafunzi kufeli mitihani yao ya kuhitimu

Muhuga ametoa agizo hilo leo katika uzinduzi wa vikao vya wadau wa elimu mkoani Katavi kwa ajili ya kujadili namna ya kuondoa vikwazo mbalimbali vinavyosababisha kiwango cha ufaulu kuendelea kuporomoka mkoani Katavi


Kwa upande wao wadau wa elimu wakiwemo wanafunzi,wazazi,walimu na viongozi kamati za shule wameshauri changamoto za uhaba wa walimu,vyumba vya madarasa na maslahi ya vitatuliwe kwa wakati ili kuongeza chachu ya ufaulu wa wanafunzi

Awali katika taarifa yake kwa mgeni rasmi,Kaimu katibu tawala mkoani Katavi Ernest Hinju Ambaye Pia Ndiye Afisa Elimu Mkoa Amesema Jumla ya vikao 7 vya wadau wa elimu vitafanyika halmashauri zote za mkoa wa Katavi na kilele cha kumalizika kwa vikao inatarajiwa kufanyika Aprili 16 mwaka huu Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Michael Nzyungu amesema Halmashauri inaendelea kutatua changamoto ya miundombinu shuleni ambapo mpaka sasa vyumba 36 vya madarasa vipo katika hatua mbalimbali za kukamilika ili kupunguza msongamano wa wamafunzi darasani na kuwa tatizo wakati wa ufundishaji na ujifunzaji

CHANZO:Isack Gerald

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...