Wakazi wa Kijiji cha Ifukutwa wilaya ya Tanganyika
Mkoa wa Katavi wameishukuru serikali kwa kupeleka huduma ya nishati ya Umeme
katika eneo hilo.
Wakizungumza na Mpana radio fm wamesema wameanza
kuona faida za nishati ya umeme kutokana na shughuri nyingi kurahisishwa na
matumizi ya nishati hiyo.
Katika hatua nyingine wameiomba serikali kuongeza
kasi ya usambazaji wa umeme kwenye makazi ya watu kutokana na zoezi hilo awali
kulenga maeneo ya huduma za jamii kama
vile Shule, vituo vya afya taasisi za kidini na ofisi za umma.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Hamad
Mapengo amesema serikali inafanya jitihada za dhati kuhakikisha wananchi
wanapata nishati ya Umeme ili kuenda sambamba na sera ya taifa ya Viwanda ili
kukuza uchumi.
Hapo jana Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania
Dk John Pombe Magufuli wakati akizindua mradi wa umeme wa Kinyerezi ameitaka
wizara ya nishati kupunguza bei ya Umeme ili kila mtanzania apate nishati hiyo
kwa urahisi.
CHANZO:Ester Baraka
No comments:
Post a Comment