Wednesday, 4 April 2018

“HAKUNA GHARAMA KUPATA KITAMBULISHO CHA TAIFA”-NIDA




Mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,imesema hakuna gharama ambazo mwananchi anatakiwa kulipia kwa ajili ya kupata kitambulisho cha taifa.

Nasra Said ambaye ni kaimu msajili wa vitambulisho hivyo wilayani Tanganyika akizungumza na Mpanda Radio amesema wananchi wanapokwenda kujiandikisha wanatakiwa wawe na nakala mojawapo kati ya kitambulisho cha Mpiga kura,cheti cha kuzaliwa au cheti cha shule.

Kauli ya NIDA imekuja baada ya wananchi wilayani Tanganyika kulalamika kulipishwa fedha kwa ajili  ya kujiandikisha huku wengine wakisema hawana elimu yoyote kuhusu vitambulisho hivyo vya taifa na kuhofia kukosa haki yao ya msingi.

Utaratibu wa kuanzisha Vitambulisho vya Taifa kwa raia wa Tanzania na wageni waishio nchini Tanzania lilianzishwa mwaka 1968 katika kikao kilichojumuisha wajumbe Kutoka nchi za Tanzania,Kenya,Uganda na Zambia.

Chanzo:Issack Gerald

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...