Friday, 6 April 2018

SERIKALI MKOANI KATAVI YAJIPANGA KUADHIMISHA MIAKA 46 YA KIFO CHA KARUME KWA KUFANYA USAFI


Serikali Mkoan Katavi imepanga kuadhimisha kumbukizi ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar  Hayati Sheikh Abeid Amani Karume kwa kufanya zoezi la usafi

Akizungumza kwa njia ya simu na Mpanda Radio msemaji wa Manispaa Pius Donald amesema zoezi watashiriki katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya  Mpanda ikiwemo Hospitali,Sokoni na Stendi kuu

Sanjari na hilo Pius ametoa wito kwa Wananchi wote kujitokeza kushiriki zoezi hilo la usafi likiwa na dhana kubwa ya  kulinda afya za watanzania

Hayati Sheikh Abeid Amani Karume ambaye alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili 1972 kwa kupigwa risasi. 

CHANZO:Ezelina Yuda

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...