Friday, 6 April 2018

WANANCHI WA KASIMBA NYUMBA ZAO ZILIZO NA ALAMA YA X WALIA NA SERIKALI JUU YA FIDIA


Wakazi wa Kasimba Kata ya Ilembo iliyopo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi waliojenga kando ya barabara ya Mpanda-Sumbawanga wameitaka Serikali kuharakisha malipo  ya fidia yao ili kupisha eneo la hifadhi ya barabara

Wakizungumza na Mpanda Radio kwa nyakati tofauti wakazi hao wamesema walikewa alama zilizoonyoshesha kuwa wangelipwa fidia tangu miaka kadhaa iliyopita na kutakiwa kutoendeleza nyumba zao lakini mpaka sasa bado hawajalipwa

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroads) mkoa wa katavi Mhandisi Antony Mwakabende amesema ni kweli TANROADS inawatambua wananchi hao lakini kutokana na ukubwa wa mtandao  wa barabara nchini  fidia italipwa pesa itakapopatikana ama kama kuna mahitaji ya upanuzi wa barabara wa wakati husika

Mhandisi Mwakabende amewaomba wananchi hao kutoacha nyumba zao kubomoka kwani wanaruhusiwa kuzifanyia marekebisho na kwamba kinachokatazwa ni ujenzi wa nyumba mpya

Kwa mujibu wa Mhandisi Mwakabende sheria ya barabara ya mwaka 2007 imeongeza upana wa barabara kutoka mita 20 hadi mita 30 kila upande

 Chanzo:Haruna Juma

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...