Friday, 16 February 2018

Wanafunzi wa shule ya sekondari Kasokola Manispaa ya Mpanda wamesema,kutokuwepo kwa somo la Teknolojia Habari na mawasiliano (Tehama) katika shule yao wanakosa mambo muhimu hasa katika matumizi ya komputa


MPANDA

Wanafunzi wa shule ya sekondari Kasokola Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamesema,kutokuwepo kwa somo la Teknolojia Habari na mawasiliano (Tehama) katika shule yao wanakosa mambo muhimu hasa katika matumizi ya komputa.

Wakizungumza na Mpanda Radio shuleni hapo wanafunzi hao wamesema,somo hilo linawatatiza wanafunzi wengi wanapofika elimu ya juu kutokana na kutojengewa msingi tangu wakiwa elimu ya chini.

Kwa upande wake kaimu mkuu wa shule ya sekondari Kasokola Mwalimu Joel Mwandwane amesema,somo la Tehama halifundishwi katika shule hiyo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ukosefu wa nishati ya umeme na somo hilo kutopewa kipaumbele kwa sasa shuleni hapo.

Shule hiyo yenye wanafunzi 415 kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne pia inakabiliwa na upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi na vyumba vya madarasa na kulazimika kwa sasa kugeuza vyumba vitatu vya maabala kutumika kama madarasa na ofisi za walimu na hivyo kuhatarisha afya za wanafunzi na walimu wao. 

Chanzo: Isack Gerald

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...