DAR ES SALAAM
Baada ya kuwepo kwa dosari kwenye uchaguzi
Jimbo la Kinondoni ikiwemo kutolewa nje kwa mawakala wa vyama mbalimbali
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni amejitokeza na kuzimaliza ambapo amewalaumu
viongozi wa vyama kushindwa kutekeleza wajibu wao.
Mkurugenzi Aron Kagurumjuli ambaye ndiye Msimamizi wa
Uchaguzi Kinondoni amesema kwamba baadhi ya vyama wameshindwa kuwapa barua za
utambulishomawakala wao na kutaka kutumia barua za kiapo kama utambulisho.
Mkurugenzi huyo amesema wao kama wasimamizi jukumu lao
lilikuwa kutoa barua hizo na pia ni jukumu la viongozi wa vyama kuhakikisha
kuwa wanatekeleza wajibu wao kwani huwa ni rahisi kwa wao kukutana na mawakala
wao kwani mpaka mawasiliano yao wanakuwa wanayo.
Aidha Mkurugenzi huyo ameweka wazi sababu za wao kutoa
barua za utambulisho saa tano usiku ni kuhofia barua hizo kugushiwa.
Hata hivyo amethibitisha kuwa dosari hizo
zimeshamalizika na hali ya vituo ni shwari hivyo wananchi wasisite kwenda
kupiga kura.
Jimbo la Kinondoni, Siha na kata nane nchini leo
yameingia katika zoezi la kupiga kura za kuchagua wabunge watakaoweza
kuwakilisha shida za wananchi wa majimbo hayo Bungeni.
Chanzo:Eatv
No comments:
Post a Comment