KATAVI.
Serikali
Mkoani Katavi imeombwa kuimarisha miradi
ya umwagiliaji sambamba na kuwachukulia hatua kali za kisheria wananchi wote
wanaoweka vizibo katika bonde dogo la mto katuma hilo Ili kukomesha uharibifu wa mazingira.
Hayo
yamesemwa na Katibu wa Jumuiya ya watumia maji bonde dogo la mto katuma Bw.
Joseph Mathius Galuka wakati akizungumza na Mpanda redio katika kata ya
Mwamkulu kufuatia shughuli mbalimbali za
kibinadamu zinazofanywa na baadhi ya wananchi katika bonde hilo na kuhatarisha
uhai wa Mto huo.
Amesema
uharibifu mkubwa hufanywa nyakati za
usiku huku baadhi ya wajumbe wa jumuiya kushindwa kufanya kazi ipasavyo
kutokana na kutishiwa maisha na wananchi waharibifu.
Baadhi
ya wananchi katika kata ya Mwamkulu wamesema kuwa shughuli za kibanadamu ndizo
zinapelekea kuhatarisha uhai wa bonde hilo na hata baadhi ya sehem maji
kukauka huku wakiwatupia lawama viongozi kwakusema wao ndio chanzo kwani huwafumbia macho wananchi waharibifu.
Ni
zaidi ya miezi 7 saba sasa tangu uongozi wa mkoa kufanya zoezi za kuzibua
vizibo katika bonde hilo dogo la mto
katuma.
No comments:
Post a Comment