Wednesday, 13 September 2017

Serikali itaendelea kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuimarisha mifumo ya udhibiti katika taasisi zake.

Makamu wa Rais, Samia Suluhu 

DAR ES SALAAM.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kuimarisha mifumo ya udhibiti katika taasisi zake.
Akizindua programu ya marekebisho ya usimamizi wa fedha za umma (PFMRP) jana Samia amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha inaboresha mfumo huo.
Samia amewahakikishia wadau wa maendeleo kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha kuwa fedha za umma zinatumika kama zilivyokusudiwa.
Awali, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema Serikali katika awamu zilizotangulia zimeonyesha mafanikio katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuongeza makusanyo ya kodi kwa kutumia mashine za kielektroniki (EFDs).
Amesema programu hiyo itatekelezwa kwa miaka mitano na itaanza kutekelezwa katika mwaka huu wa fedha (2017/18) hadi
mwaka 2021/22.

@habari na Mwananchi .

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...