Wednesday, 30 August 2017

Mpanda: Madereva wa bodaboda wametakiwa kujisajili katika vituo vya magesho.



Madereva wa bodaboda  katika Halmashauri ya manispaa ya mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kujisajili katika vituo vya magesho kama agizo la Sumatra ili kupunguza matukio ya uhalifu.
Hayo yameelezwa na askari usalama barabarani mkoa wa kativi John Shindika wakati wakizungumza na Mpanda Redio  na kusema kuwa matukio mengi yanatokea pale ambapo waendesha bodaboda wanakuwa hawafahamiani wao kwa wao.
Shindika amesema madhara wanayoyapata madereva bodaboda kutoka na uhalifu unaofanywa na watu wasiojulikana ni pamoja na kupoteza maisha kujeruhiwa na wakati mwingine kunyweshwa madawa ya kulevya na kutupwa maeneo hatarisha wakiwa hawajitambui.

hata hivyo ametoa wito kwa madereva wote kuzingatia kanuni za kazi zao ikiwemo kuvaa kofia ngumu  kutoongea na simu pamoja na kuacha kuendesha kwa mwendo kasi hali ambayo itapunguza ajali za barabarani.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...