GEITA.
Polisi wametumia mabomu ya machozi
kuwatawanya wananchi na madiwani waliofunga barabara ya kuingia kwenye
Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).
Katika tukio hilo leo, madiwani wawili
na baadhi ya wananchi wamekamatwa na polisi.
Madiwani wa halmashauri mbili za Wilaya ya Geita jana
Jumatano walitanga mgogoro na GGM wakishinikiza kulipwa Dola 12 milioni za
Marekani zinazotokana na ushuru wa huduma kuanzia mwaka 2004 hadi 2013.
Walitangaza kuzuia magari ya mgodi
kwa kufunga barabara na
pia kufunga maji yanayoingia mgodini kutoka Ziwa Victoria.
Polisi hivi sasa wameimarisha ulinzi
kwenye maeneo ya Nungwe uliko mradi wa kusambaza maji mgodini, eneo la uwanja
wa ndege na geti la kuingia mgodini.
Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi
na mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma wameingia mgodini baada ya
madiwani na wananchi kutawanywa.
No comments:
Post a Comment