Serikali
ya kijiji cha Songambele Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi
imesema,inachukua hatua za haraka kuhakikisha inakarabati visima vya maji
vilivyoharibika.
Mwenyekiti
wa kijiji hicho Bw.Beato Kambimbaya amesema,muda wowote huduma ya maji itakuwa
vizuri kwa kuwa fedha za kukarabati wa visima ipo na kinachosubiriwa ni
kuidhinishiwa matumizi.
Aidha
amesema halmashauri inaendelea kuchunguza usalama wa maji yanayotumiwa na
wakazi wa kijiji cha Songambele ili kubaini usalama wake.
Hivi
karibuni wakazi wa kijiji cha Songambele walilalamikia tatizo la mabomba ya
maji kuharibika mara kwa mara huku baadhi ya wananchi wakihofia baadhi ya
visima kutokuwa na maji safi na salama.
Kijiji cha
Songambele chenye zaidi ya wakazi elfu nne,kwa sasa kina visima vitano huku
vitatu kati ya hivyo ndivyo vinavyotumiwa na wakazi.
No comments:
Post a Comment