Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika
Salehe Muhando amewataka wakazi wanaoishi katika maeneo yasiyo rasmi kwa makazi
yakiwemo Kalumbi,Migengebe na Kidongo Chekundu kuondoka katika maeneo hayo kabla
ya Julai 18 mwaka huu.
Muhando ametoa wito huo katika
ziara ambayo ameifanya katika kata ya Katuma kwa ajili ya kuelimisha wananchi
katika masuala mbalimbali ikiwemo utunzaji wa mazingira katika msitu wa Tongwe
Magharibi unaozungukwa na vijiji 11 kati ya 55 vya wilaya hiyo.
Aidha Muhando amemwagiza Mkuu
wa Kituo cha Polisi Kata Katuma Chilongo Fwele,kuwakamata wananchi wanaoendelea
kuharibu chanzo cha maji cha mto Katuma kwa kufanya shughuli za kibinadamu
zinazokiuka umbali wa mita 60 kutoka chanzo cha mto
Hata hivyo baadhi ya viongozi
wa kata ya Katuma wameshauri udhibiti wa watu wanaoharibu mto Katuma ufanyike
kwa maeneo yote yanayozunguka mto huo.
No comments:
Post a Comment