Na;Neema Husein
Shule ya sekondari Mwangaza iliyopo Manispaa ya Mpanda mkoani
Katavi inakabiliwa na changamoto mtaalam wa maswala ya maabara licha ya kuwepo na vifaa vya kutosha.
Hayo yamebainishwa na
mkuu wa shule hiyo Simeon Lubange wakati akizungumza na Mpanda Radio ofisini
kwake na kusema kuwa walimu wa masomo ya sayansi inawaradhimu kuchukua jukumu
la mtaalam huyo.
Aidha amewataka
wanafunzi wa shule hiyo kutumia fursa
vizuri ya kuwepo kwa maabara ya masomo matatu ya sayansi shuleni hapo.
Hata hivyo ameiomba
serikali kutatua tatizo hilo mapema kwa kuleta wataalam wa maswala ya maabara
katika shule ambazo hazina wataalam hao.
No comments:
Post a Comment