Na;Restuta Nyondo
Wananchi wa Wilaya ya
Mpanda wametakiwa kujitoa katika kushiriki katika kuchangia miradi mbali mbali
ya maendeleo hususani sekta ya elimu na afya.
Mkuu wa wilaya ya
Mpanda Lilian Charles Matinga akizungumza na Mpanda radio ofisin kwake Amesema
kuwa mwamko wa wananchi katika kuchangia maendeleo bado ni mdogo hali
inayopelekea kuchelewesha maendeleo.
Matinga ametoa wito kwa wazazi kujitoa katika
kuchangia chakula mashuleni ili kuboresha afya za wanafunzi na kuongeza ufanisi
katika taaluma.
Ni wajibu wa mwananchi
kuchangia asilimia 20 ya maendeleo na serikali kuchangia asilimia 80.
No comments:
Post a Comment