Na;Rebeka Kijja
Baadhi ya wananchi katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamelalamikia utaratibu
uliowekwa katika zoezi la kujiandikisha vitambulisho vya uraia.
Wamesema hayo wakati
wakizungumza na Mpanda Radio kwa nyakati tofauti ambapo wameeleza kuwa maelezo
wanayopewa na wasimamizi wa zoezi hilo bado hayajakidhi uhitaji wao hali ambayo
inawafanya waone ugumu katika kukamilisha zoezi.
Katika hatua nyingine wazee na
watu wenye ulemavu wameiomba serikali kuwaangalia kwa ukaribu kwani zoezi kwao
linakuwa gumu hali inayowafanya wajione kama wametengwa katika zoezi hilo.
Wazo la kuanzisha Vitambulisho
vya Taifa kwa raia wa Tanzania na wageni waishio nchini Tanzania lilizaliwa
mwaka 1968 katika kikao cha “Interstate Intelligence Gathering” kilichojumuisha
wajumbe Kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda na Zambia ambapo iliazimiwa
kwamba ili kuimarisha mahusiano ya kiusalama yanayozingatia Utawala wa Sheria
katika nchi hizo nne
No comments:
Post a Comment