Na:Haruna Juma
Baadhi ya vijana waliokuwa
wakiosha magari katika Mto mpanda eneo la Misunkumilo wameiomba Manispaa ya
Mpanda kuwatengea eneo lingine la kufanyia shughuli hiyo baada ya kuwatimua
kutoka Mto huo.
Wakizungumza na mpanda Radio
vijana hao wamesema kwa muda mrefu sasa vijana wengi wamekuwa wakijipatia
riziki kutokana na shughuli hiyo
Wamesema uongozi wa manispaa
ulipaswa kutafuta mbinu mbadala ya kuwaondoa mtoni badala ya njia iliyotumika
ambayo wamesema inaweza kuleta madhara kwa jamii nzima.
Halmashauri ya Manispaa ya
Mpanda imepiga marufuku shughuli za kuosha magari katika vyanzo vya maji ili
kutunza mazingira na vyanzo vya maji
No comments:
Post a Comment