Wakazi wa kata ya Katuma
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,wameiomba serikali kuwaondoa
viboko katika makazi ya watu
Wakizungumza katika Mkutano wa
hadhara katika kijiji cha Katuma wamesema
kwa sasa viboko wanazagaa maeneo ya Zahanati ya Katuma na kula mazao
shambani
Kaimu Afisa ardhi na maliasli
wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Elisha Mengele,amekiri kupata taarifa za
kuzagaa wanyama hao kutoka mto Katuma na kuwataka wananchi kutoa taarifa sahihi
na ushirikiano
Wakazi wa wilaya ya Tanganyika
na Mpanda wanaozunguka mto Katuma wamkuwa wakilalamika mazao yao kuvamiwa na
viboko hao ambapo kwa mjibu wa Bw.Mengele viboko huhama katika maeneo yao msimu
wa masika.
No comments:
Post a Comment