Mkuu wa Wilaya ya
Tanganyika Mkoani Katavi Salehe Muhando,amesema wizara ya maliasili na utalii
imekubali msitu wa Tongwe Magharibi kumilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya
Mpanda kutoka katika mamlaka ya wizara hiyo.
Muhando amebainisha
hatua hiyo kupitia mikutano ya hadhara katika vijiji vya Kapanga na Katuma Kata
ya Katuma lengo likiwa ni kuelimisha kutunza msitu huo wenye zaidi ya sokwe 800
kwa ajili ya faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mpanda Mh.Hamadi Mapengo amesema
mchakato wa kuomba kumiliki msitu huo ulianza mwaka 2002 ambapo kwa sasa
kutaongezeka mapatao yatokanayo na msitu ikiwa ni pamoja na kupata watalii kwa
ajili ya kuja kuwaona wanyama.
Kwa mjibu wa Kaimu wa
afisa ardhi na maliasili wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Elisha
Mengele,vijiji vipatavyo 11 vinavyozunguka msitu huo vikiwemo
Kapanga,Lugonesi,Katuma,Mpembe na Tongwe vinatarajia kunufaika zaidi na msitu
huo.
No comments:
Post a Comment