Wajasiriamali
wanaojishughulisha na uzalishaji wa
Asali katika mkoa wa Katavi wameshauriwa kuzalisha bidhaa hiyo kwa kuzingatia
uwekaji wa alama Tambuzi yaani bakodi na kwa kuzingatia viwango vinavyo tambuliwa na shirika la
kudhibiti ubora wa bidhaa Tbs.
Hayo yamebainishwa na
kaimu katibu Tawala mkoa wa Katavi Wilbad Marandu wakati akifungua semina ya
wazalishaji wa bidhaa hiyo yanaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Idara
ya maji manispaa ya Mpanda.
Pia amesema bidhaa
nyingi zitokanazo na nyuki zimekuwa zikizalishwa pasipo kuwekewa alama Tambuzi
hali ambayo huwakosesha fursa ya bidhaa hiyo kuuzika kimataifa.
Kwa upande wake mwakilishi
wa shilika la kizibiti ubora wa bidhaa Tanzania tbs kutoka mikoa ya nyanda za
juu kusini Abeli Clement amaesema jukumu
kubwa la la shilika hilo nikuhakikisha bidhaa zinazo zalishwa zipo katika
kiwango kinacho kubalika.
No comments:
Post a Comment