Mkuu wa Wilaya ya
Mpanda Lilian Charles Matinga amewataka wananchi kutunza miradi ya maji ambayo
imezinduliwa na mwenge wa uhuru ili iweze kutumika kwa malengo husika.
Ameyasema hayo wakati
akizungumza na Mpanda Radio ofosini kwake na kusema kuwa miradi iliyozinduliwa
yote imeshaanza kutumika hususani miradi ya visima vya maji na kuwataka
wananchi kuunda kamati za maji ili kuindeleza miradi hiyo.
Aidha amesema kuwa
utunzaji wa miundominu ni wajibu wa
jamii nzima ikisimamiwa na kamati ya watumia maji.
Mei 2 mwaka huu Mwenge
wa uhuru katika halmashauri ya manspaa ya Mpanda ulizindua miradi 10 ya maendeleo yenye thamani ya
shilingi milioni 800 ikiwemo miradi ya Kisima cha maji,zahanati ya Milala,klabu
za kupambana na rushwa,mimba za utotoni pamoja na madawa ya kulevya.
No comments:
Post a Comment