Jeshi la Polisi mkoani Katavi
limewataka wananchi kutoa tarifa ya vitendo vya utapeli kwa njia ya simu za
mkononi.
Hayo yamesemwa na kaimu
kamanda wa polisi mkoa wa Katavi Benedict
Mapugila alipokuwa akihojiwa kwa njia ya simu mapema leo, ambapo amekili
kuwepo kwa vitendo hivyo, na kuwataka wananchi kutofuata maelekezo yanayotolewa na matapeli kwanjia ya
ujumbe mfupi.
Kuenea kwa ujumbe huo ambao
hutoa maelekezo namna ya kutuma fedha
kwenye namba nyingine ambayo
huambatanishwa kumezua hofu kubwa miongoni mwa jamii, huku wangine wakikosoa
kuhusu udahifu wa mitandao hiyo juu ya kupambana na suala hilo.
Nisiku moja tu tangu msemaji
wa Jeshi la polisi nchini Barnabas Mwakalukwa kuutadharisha umma juu ya vitendo
hivyo.
No comments:
Post a Comment